Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF YAUNGA MKONO JUHUDI ZA KUIMARISHA AFYA KWA KUSHIRIKI NBC MARATHON

PSSSF YAUNGA MKONO JUHUDI ZA KUIMARISHA AFYA KWA KUSHIRIKI NBC MARATHON

News
News

Dodoma, 26/07/2026

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeshiruki kikamilifu katika Mbio za NBC Marathon zilizofanyika katika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma, kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za kuhamasisha afya na kuimarisha ushirikiano na jamii.


Mbio hizo zilizokusanya mamia ya washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi zilijumuisha masafa ya kilometa 42, kilometa 21, kilometa 10 pamoja na kilometa 5.


Mgeni Rasmi katika tukio hilo alikuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB) ambaye aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Rosemary Senyamule, pamoja na viongozi wengine wa serikali na taasisi mbalimbali.

Baadhi ya Watumishi wa PSSSF walioshiriki mbio za kilomita 42 (Full Marathon), Ndugu Mohamed Nyalo (kushoto) na Twasini Athumani (kulia), wakiiwakilisha Mfuko katika NBC Dodoma Marathon 2026.

Watumishi na viongozi wa PSSSF walishiriki katika mbio hizo kwa kukimbia katika masafa tofauti, hatua inayolenga kuhamasisha mtindo bora wa maisha kupitia michezo na mazoezi ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Akizungumza wakati wa ufunguzi na utoaji wa zawadi, Mgeni Rasmi, alipongeza taasisi zote zilizoshiriki, ikiwemo PSSSF, kwa kujitokeza kwa wingi na kuunga mkono michezo yenye tija kwa afya na maendeleo ya jamii.

Baadhi ya Watumishi wa Mfuko katika mbio hizo

Bi. Rehema Mkamba Mtumishi wa PSSSF (katikati) akiwasilisha Mfuko mbio za Kilomita 21 wakati wa mbio za Mbio za NBC Marathon, 2026

Tukio hilo lilimalizika kwa amani na shamrashamra huku washiriki wakitunukiwa medali.