PSSSF YASHIRIKI CRDB MARATHON 2026
Dar es Salaam, Agosti 16, 2026
Watumishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wamshiriki CRDB Marathon 2026 zilizofanyika Agosti 16, 2026, ambapo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya CCBRT zilipokea jumla ya Shilingi milioni 200 kama mchango kutoka kwenye mapato ya mbio hizo kwa lengo la kusaidia huduma mbalimbali za tiba katika taasisi hizo za tiba.

Meneja wa Mfuko wa PSSSF wa Kanda ya Ilala Bi. Amina Kassim akiwa ameambatana na Afisa Uhusiano na Elimu kwa Wanachama Bi. Regina Khumba wakiwa katika ushiriki wa CRDB Marathon 2026 jijini Dar es Salaam
Mbio hizo zilianzia na kuishia katika Viwanja vya Posta Kijitonyama, jijini Dar es Salaam na kuhusisha watu mbalimbali ambao walishiriki mbio za kilomita 5, kilomita 10, kilomita 21, kilomita 42, pamoja na mbio maalumu za baiskeli za kilomita 65.

Picha ya pamoja ya baadhi ya Watumishi wa Mfuko wa PSSSF walioshiriki CRDB Marathon tarehe 16 Agost, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Lengo la mbio hizo ni kuhamasisha jamii kushiriki katika michezo na mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya, zimekuwa jukwaa muhimu la kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi mara kwa mara, kuzingatia lishe bora, na kuchukua hatua za mapema katika kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

Picha ya pamoja ya baadhi ya Watumishi wa Mfuko wa PSSSF walioshiriki CRDB Marathon tarehe 16 Agost, 2026 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa CRDB Marathon katika mbio hizo