Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Apongeza Huduma za Kidijitali na Uwekezaji wa Mfuko PSSSF

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Apongeza Huduma za Kidijitali na Uwekezaji wa Mfuko PSSSF

News
News

Mbeya, Agosti 3, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere, ametembelea banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayoendelea Viwanja vya John Mwakangale, mkoani Mbeya, ambapo amepongeza juhudi za Mfuko huo katika kuunga mkono kauli mbiu ya Nanenane 2026, "Tambua Soko, Ongeza Tija kwa Kutekeleza DIRA 2050," kupitia huduma za kidijitali zinazorahisisha upatikanaji wa huduma na maombi ya mafao kwa wanachama na wastaafu, hivyo kuwawezesha kutumia muda wao zaidi katika shughuli za kukuza uchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere, ametembelea banda la Mfuko wa PSSSF kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 3, 2026

Katika ziara hiyo, Mhe. Nyerere pia alijionea bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha Ngozi cha KLICL, moja ya uwekezaji wa Mfuko, ambao umechangia kuongeza ajira, kuimarisha soko la ngozi kwa wafugaji na kuongeza thamani ya mazao ya mifugo kupitia uzalishaji wa bidhaa za ngozi kama viatu, mikanda, pochi na mifuko.

Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Mhe. Nyerere alisema, "ingependa kuona huduma hizi za kidijitali pamoja na bidhaa za Kiwanda cha Ngozi cha KLICL zikiletwa Mkoa wa Rukwa wakati wa kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu, ili wananchi wa mkoa wetu nao wapate fursa ya kunufaika na huduma hizi na kujionea bidhaa zinazozalishwa na uwekezaji wa PSSSF," alisema Mhe. Nyerere.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere akishuduhudia bidhaa za Ngozi zinazotenlenezwa na Kiwanda cha Ngozi cha KLICL

Huduma zikitolewa Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, jijini Mbeya

Mkuu wa Mkoa huyo alipokelewa na Afisa Mahusiano na Mawasiliano Mkuu wa Mfuko wa PSSSF Bi. Queen Edward, ambaye alimshukuru kwa kutembelea banda hilo na kuahidi kuwa Mfuko utashiriki Mkoani Rukwa katika kilele cha mbio za Mwenge .