HONGERENI PSSSF KWA KUELIMISHA WANA HABARI
Shinyanga, Septemba 18, 2026
Wanachama wa klabu za Waandishi wa habari wa mikoa ya Shinyanga (SPC), Simiyu (SMPC) na Mtandao wa wana blogu Tanzania (TBN) mkoani Shinyanga wameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuandaa semina ambayo imewaongezea uelewa juu ya huduma na mafao yatolewayo na PSSSF.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Bw. Greyson Kakuru, akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo iliyohudhuriwa na wanachama wa SPC, SMPC na TBN kutoka mikoa hiyo alisema, semina elimu waliyoipata imewapa uelewa mpana utakaowasaidia kufikisha habari kwa usahihi.
“ Ninawashukuru sana PSSSF kwa uamuzi huu kwetu sisi waandishi wa habari." Alisema.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Bw. Greyson Kakuru akizunguza wakati wa ufunguzi wa semina kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Shinyanga, Simiyu na wanachama wa Tanzania Bloggers Network.
Naye Mwenyekiti wa TBN Shinyanga, Bw. Kadama Malunde, mafunzo hayo yatawasaidia kutengeneza maudhui ambayo yatasaidia kuandaa habari kwa usahihi kwa lengo la kuwafikishia wanachama wa PSSSF na watanzania kwa jumla.

Baadhi ya washiriki wa semina ya waandishi wa habari wa mikoa ya Shinyanga, Simiyu na wanachama wa Tanzania Bloggers Network iliyoandaliwa na PSSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
Aidha, Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Simiyu, Bw. Paschal Michael alisema, mafunzo haya yamewaleta pamoja wanachama wa klabu hizo kutoka Mikoa hiyo mitatu na hivyo yatakenga Mahusiano mema na MAAFISA wafawidhi wa PSSSF kwenye Mikoa hiyo kwa lengo la kutoa taarifa sahihi kuhusu Mfuko.

Mmoja wa washiriki wa semina kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Shinyanga, Simiyu na wanachama wa Tanzania Bloggers Network akiuliza swali wakati wa semina hiyo.
Kwa upande wake, Afisa Uhuasiano wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi alisema,
“Semina hizi zipo katika mpango kazi wa PSSSF wa kuwafikia wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, kwa lengo la kutoa elimu ili muweze kuelimisha umma kwa usahihi juu ya huduma na mafao yanayotolewa na PSSSF.