MILIONI 30 ZA PSSSF KUOKOA VICHANGA MWANZA
Mwanza, Novemba 17, 2026
Na Mwandishi Wetu,
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umepeleka tabasamu mkoani Mwanza baada ya kukabidhi vifaa tiba vya kuokoa maisha ya watoto wachanga vyenye thamani ya Shilingi Milioni 30 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure. Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo katika maadhimisho ya watoto waliozaliwa kabla ya muda.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Daktari Mfawidhi wa Hospitali ya Sekou Toure, Bi. Bahati, aliwapongeza wauguzi na wafanyakazi kwa kupambana mchana na usiku kuwahudumia watoto, huku akishukuru msaada huo wa PSSSF ambao utafanikisha mapambano yao katika kuokoa afya ya watoto wachanga.

Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki, Bw. Rajab Kinande akikabidhi zawadi kwa kina mama wenye watoto wachanga katika hospitali ya Sekou Toure katika hafla ya Maadhimisho ya watoto waliozaliwa kabla ya muda ambapo PSSSF ilikabidhi msaada wa vifaa kwaajili ya kusaidia watoto wachanga katika Hospitali hiyo.
Naye Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki, Bw. Rajab Kinande, alisisitiza kuwa PSSSF inashirikiana na Serikali kupeleka misaada kwenye maeneo yenye uhitaji ili kuwezesha watoto wanaishi na kulifaa Taifa, akitoa wito kwa hospitali hiyo kutunza vifaa hivyo vizuri.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa, Bw. Hery Kagya, alisema kuwa Mwanza ina wanawake zaidi ya 900,000 wenye umri wa kujifungua, hivyo msaada huo wa vifaa kutoka PSSSF ni ukombozi mkubwa kwa watoto njiti na wenye uzito uliopungua.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Kheri Kagya (mwenye shati ya drafti) kushoto ni Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki, Bw. Rajab Kinande wakiwa na kina mama waliojifungua watoto kabla ya muda wakiwa
Furaha hiyo ilionekana wazi kwa Bi. Annamaria George, ambaye alitoa neno kwa niaba ya wazazi na kueleza kwa furaha jinsi mwanae alivyozaliwa na uzito wa gramu 600 tu, lakini kupitia madaktari bingwa na msaada huo wa PSSSF, mtoto huyo sasa ana uzito wa kilo moja na gramu 500.
Vifaa vilivyokabiadhiwa ni; mashine ya Bubble CPAP, Patient Monitor, heater za ndani pamoja na vifaa vingine vinaosaidia katika vyumba wanavyotunziwa watoto wachanga.