BUNGE: PSSSF TOENI ELIMU KWA WATUMISHI WAPYA KAZINI
Dodoma, Oktoba 16, 2026
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii imeushauri Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuongeza kasi ya utoaji wa elimu ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wapya wanaoajiriwa katika Utumishi wa Umma, ili kuwajengea uelewa wa haki, wajibu na umuhimu wa kujiandaa na maisha ya kustaafu tangu wanapoanza ajira.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Hawa Mchafu akizungumza wakati wa kikao cha Kamati hiyo, Bungeni Jijini, Dodoma
Ushauri huo umetolewa wakati wa kikao kati ya PSSSF na kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma za jamii, wakati PSSSF ilipokuwa ikiwasilisha taarifa ya utekelezaji mbele ya kamati hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii leo tarehe 16/10/2026 Bungeni, Dodoma

Mhe. Kafiti William Kafiti Mbunge wa Jimbo la Ilemela (Katikati) akiwa kikaoni wakati wa kikao cha wa kikao cha Kamati hiyo, Bungeni Jijini, Dodoma
Akichangia katika kikao hicho, mjumbe wa Kamati hiyo kutoka Jimbo la Ilemela, Mhe. William Kafiti, alisema, “ni muhimu wa elimu hiyo kutolewa kwa watumishi tangu hatua za awali za ajira zao, ili waweze kuelewa mfumo wa hifadhi ya jamii, michango yao, mafao wanayostahili pamoja na namna ya kufanya maandalizi ya maisha baada ya kustaafu.”
Mhe. Kafiti alilisitiza kuwa kuimarishwa kwa elimu kwa wanachama kutasaidia kuongeza uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko na kuwawezesha watumishi kufanya maamuzi sahihi kuhusu mustakabali wao wa kifedha wakati wa utumishi na baada ya kustaafu.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Fortunatus Magambo akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii leo Bungeni, jijini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu aliwasilisha taarifa ya utendaji wa Mfuko katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii leo tarehe 16/10/2026 Bungeni, Dodoma
Awali, akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Mfuko hadi kufikia Septemba 2026, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema PSSSF imeendelea kuimarika katika utoaji wa huduma, uwekezaji na usimamizi wa mafao, huku thamani ya Mfuko ikifikia shilingi trilioni 16. Ameeleza kuwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yamechangia kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wanachama na wastaafu, kurahisisha taratibu za huduma na kuwezesha malipo ya mafao kufanyika kwa wakati.

Mhe. Kangi Lugola, Mb akichangia hoja wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, leo tarehe 16/10/2026
Aidha, wajumbe wa Kamati wamesisitiza umuhimu wa PSSSF kuendelea kuimarisha elimu kwa wanachama sambamba na kuongeza uwekezaji wenye tija unaochochea fursa za ajira nchini.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSSSF Bw. Hajji Khamis, akitoa ufafanuzi wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii leo tarehe 16/10/2026 Bungeni, Dodoma
Katika hatua nyingine, wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kusimamia sekta ya hifadhi ya jamii nchini, pamoja na juhudi za Serikali za kulipa deni lake kwa Mfuko ili kuimarisha uwezo wake wa kutekeleza majukumu.
.