SANGU: Michango ya Wanachama PSSSF inawekezwa na kurejesha faida
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sangu, amesema uwekezaji wa PSSSF kwenye mradi wa Rock City Mall jijini Mwanza ni thibitisho kwamba michango ya wanachama inalindwa, inakua na kurejesha faida.

Mhe. Deus Sangu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri wa Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi gawio kutuka kampuni ya Mwanza Rockycity, kampuni inayoendesha mradi wa Mwanza Rockcity Mall, Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma, katika Ukumbi wa mikutano wa PSSSF.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma wakati Kampuni ya Mwanza Rock City Ltd ikitoa gawio la jumla ya TZS bilioni 1.18 kwa wabia wake watatu. Katika gawio hilo, PSSSF ambaye ni muwekezaji mkuu imepokea TZS bilioni 1.7 (90%) Halmashauri ya Jiji la Mwanza (6%) imepokea TZS milioni 71.3 na Manispaa ya Ilemela imepokea TZS milioni 47.56 (4%).
Mhe. Sangu amempongeza Bodi na Menejimenti ya PSSSF chini ya Mkurugenzi Mkuu Bw. Fortunatus Magambo kwa usimamizi mzuri unaowezesha mafanikio haya, "niwapongeze kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuhakikisha michango ya wanachama inalindwa, inakua na kurejesha faida kwa Taifa. Leo hatupokei gawio tu, tunapokea uthibitisho kuwa Mfuko wetu wa hifadhi ya jamii uko imara, unakua na unalipa.” Alisema Mhe. Sangu.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Fortunatus Magambo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mwanza Rockcity, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi gawio kutuka kampuni ya Mwanza Rockycity, kampuni inayoendesha mradi wa Mwanza Rockcity Mall, Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma, katika Ukumbi wa mikutano wa PSSSF.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo, ameeleza kuwa lengo kuu la uwekezaji huu ni kulinda thamani ya michango ya wanachama ili wanapostaafu waweze kulipwa mafao kwa wakati, amelinganisha tukio hilo na siku ya mavuno. “Hakika ile mbegu tuliyopanda, ilimea vyema na hatimaye leo tunavuna tulichopanda, hakika leo ni siku muhimu sana.” Alisema Bw. Magambo.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza. Mhe. Sima Constatine Sima akitoa shukrani kwa kampuni ya Mwanza Rockcity Limited wakati wa hafla ya kukabidhi gawio kutuka kampuni ya Mwanza Rockycity, kampuni inayoendesha mradi wa Mwanza Rockcity Mall, Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma, katika Ukumbi wa mikutano wa PSSSF.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Constantine Sima, Meya wa Ilemela Mhe. Sarah Ng’wani, Mbunge wa Ilemela, Kafiti William Kafiti na Mbunge wa jimbo la Nyamagana, Mhe. John Nzilanyingi, madiwani, menejimenti ya PSSSF na bodi ya Mradi huo.

Meneja wa Mradi, Bi Aneth Shoo akitoa taarifa ya utendaji wa Mradi huo katika hafkla hiyo.
Mradi huo wa Rock City Mall, asilimia 98 ya jengo lina wapangaji ambapo Meneja wa Mradi huo, Bi. Aneth Shoo alisema Mradi huo umekua ni nembo ya kutambulisha jiji la Mwanza, unapendezesha Jiji, kusogeza huduma na kutoa ajira za kudumu kwa watu 1,007.


Mhe. Deus Sangu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri wa Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, katika picha ya pamoja na madiwani wa Jiji la Mwanza baada ya kupokea gawio kutoka kwa Kampuni ya Mwanza Rockcity Limited, hafla iliyofanyika Jijini Dodoma