Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF yashiriki Mkutano wa TEF, yapokea na kutoa tuzo

PSSSF yashiriki Mkutano wa TEF, yapokea na kutoa tuzo

News
News

Morogoro, Novemba 26, 2026

Na Mwandishi wetu,

Watumishi wa PSSSF wameshiriki mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ambapo amesisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari kwa kuwa ni wadau muhimu katika maendeleo na mshikamano wa taifa.

Katika hotuba yake, Dkt. Mwigulu amehimiza umuhimu wa umoja wa kitaifa na kujenga mtazamo chanya kwa sekta binafsi ili kukuza uchumi.

“Kujenga umoja wa kitaifa ni kazi endelevu isiyopaswa kuachwa, na tunapoelekea kwenye malengo makubwa ya kiuchumi na kuzalisha ajira nyingi, hatuna njia mbadala lazima tujenge sekta binafsi iliyo imara na inayoheshimika,” amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akikabidhi tuzo kwa Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Bw. Omega Ngole katika Mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF). Tuzo hiyo imetolewa na TEF kwa PSSSF kutambua mchango wake katika kufanikisha mkutano huo.

Katika mkutano huo, PSSSF ilipokea cheti pamoja na tuzo kutoka TEF zilizokabidhiwa na Waziri Mkuu kutambua mchango wa Mfuko kufanikisha mkutano huo.

Aidha, PSSSF ilikabidhi tuzo kwa TEF kuthamini ushirikiano na mchango wake chanya kwa Mfuko katika kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu hifadhi ya jamii.

Meneja Daftari la Wastaafu, Bw. Victor Kikoti akiwasilisha mada ya Mfuko katika mkutano mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)

Kwa upande wake, Meneja wa Daftari la Wastaafu wa PSSSF, Bw. Victor Kikoti, alitoa mada ambapo alihimiza wanachama kuwashirikisha watu wanafamilia taarifa muhimu, na pia kukagua na kuboresha taarifa zao ili kuwezesha malipo ya mafao yao kufanyika kwa wakati.