Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF YAENDESHA SEMINA KWA MAAFISA UTUMISHI MARA.

PSSSF YAENDESHA SEMINA KWA MAAFISA UTUMISHI MARA.

News
News

Na Mwandishi Wetu,

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeendesha semina kwa Maafisa Utumishi Mkoa wa Mara, ili kuwajengea uelewa wa kushughulikia kwa weledi masuala ya wanachama wa mfuko huo.

Semina hiyo imefanyika Ijumaa Novemba 06, 2026 katika Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara ambapo washiriki wa semina hiyo wamehimizwa kuwasaidia wanachama wa PSSSF kupata huduma bora na kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Brigedia Jenerali Evans A. Mtambi Akizungumza wakati wa Kufungua Semina ya mafunzo kwa Waajiri, Leo Novemba 6, 2026.

Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mara Brigedia Jenerali Evans A. Mtambi amesema semina hiyo pia itasaidia kuongeza ufanisi katika upatikanaji wa huduma za PSSSF hususani matumizi ya huduma za kidigitali kwa wanachama.

“Zamani mtu alikuwa anafunga safari kwenda Dar es salaam, Dodoma au makao makuu ya Mkoa, lakini sasa hivi anawasha tu bando kwenye simu yake, anawasilisha hitaji lake na anahudumiwa akiwa nyumbani” amesema RC Mtambi.

Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki, CPA. Rajabu Kinande akizungumza katika Semina ya Mafunzo kwa Maafisa Utumishi, Leo Novemba 6, 2026.

Naye Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki, CPA. Rajabu Kinande amesema ili kuhakikisha Mfuko huo unatoa huduma bora na ya haraka, umejikita kuwafikia wanachama wake kwa njia ya kidigitali.

“Sasa hivi mteja anaweza kupata huduma kupitia simu yake ya mkononi hivyo ili kuhakikisha huduma hiyo inaenda vizuri tukaona ni vyema kukutana na maafisa Utumishi ambao wana wajibu wa kutusaidia kutoa huduma bora kwa wanachama” amesema CPA. Kinande.

Maafisa Utumishi wakiwa katika Semina ya Mafunzo iliyoandiwa PSSSF, Leo Novemba 6, 2026.

Akitoa shukurani kwa niaba ya Maafisa Utumishi mkoani Mara, Jumanne Obogo ambaye ni Afisa Utumishi Halmashauri ya Musoma Vijijini amesema semina hiyo itawasaidia kuwahudumia kwa ufanisi watumishi kupitia mfumo wa kidigitali.