Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF YATOA ELIMU YA HUDUMA ZAKE KWA WIZARA YA MAJI

PSSSF YATOA ELIMU YA HUDUMA ZAKE KWA WIZARA YA MAJI

News
News

Dodoma, 17 Novemba 2026

Na Mwandishi wetu,

PSSSF imetoa elimu ya Mfuko kwa watumishi wa Wizara ya Maji ambao ni maofisa Utawala na Rasilimaliwatu, Maendeleo ya Jamii pamoja na Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma.


Elimu hiyo ilitolewa na timu ya PSSSF iliyoongozwa na Meneja wa Kanda ya Kati, Dodoma, Bw. Lulyalya Sayi leo, tarehe 17 Novemba, katika Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF jijini Dodoma.

Meneja wa PSSSF, Kanda ya Kati, Dodoma, Bw. Lulyalya Sayi akitoa elimu kwa watumishi wa Wizara ya Maji ambao ni maofisa Utawala na Rasilimaliwatu, Maendeleo ya Jamii pamoja na Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wakati wa Mkutano wao unaendelea kuanzia tarehe tarehe 17 - 19 Novemba, katika Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF jijini Dodoma.

Akizungumza katika mkutano huo, Bw. Sayi aliwasisitiza washiriki kuhakikisha michango ya wafanyakazi inawasilishwa kwa wakati na taarifa za wanachama zinasafishwa mara kwa mara, ili wanachama waweze kupata mafao yao kwa wakati pale yanapostahili.

Afisa Matekelezo wa PSSSF, Bw. Frank Fute, aliwaelimisha wataalamu hao kuhusu matumizi ya huduma za kidijitali wakati wa seminan hiyo inayoendelea jijini Dodoma

Maafisa wa PSSSF, wakiongozwa na Meneja wa PSSSF, Kanda ya Kati, Dodoma, Bw. Lulyalya Sayi, wa kwanza kulia pamoja na maafisa wengine, Noel Sabugo Afisa Matekelezo wa PSSSF, Bi. Esther Mpemba na Bi. Consolata Lukuvi kutoka idara ya matekelezo, wakiwa katika mkutano huo wa watumishi wa Wizara ya Maji.

Kwa upande wake, Afisa Matekelezo wa PSSSF, Bw. Frank Fute, aliwaelimisha wataalamu hao kuhusu matumizi ya huduma za kidijitali, hususan mifumo ya PSSSF Member Portal na PSSSF Kiganjani. Alieleza kuwa mifumo hiyo imesaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wanachama, kwa kuwawezesha kupata huduma na taarifa zao kwa urahisi na kwa wakati popote walipo.

Watumishi wa Wizara ya Maji ambao ni maofisa Utawala na Rasilimaliwatu, Maendeleo ya Jamii pamoja na Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wakati wa Mkutano

Timu ya PSSSF ilieleza kwa kina huduma zinazotolewa na Mfuko pamoja na mafao mbalimbali kwa wanachama, na kuwajengea washiriki uelewa utakaowawezesha kuwahudumia vyema watumishi wa sekta ya maji katika taasisi zao. PSSSFSSSF itaendelea kutoa elimu kwa wadau na wanachama wake ili kuhakikisha wanapata huduma bora na kuelewa haki zao.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maji ambao ni maofisa Utawala na Rasilimaliwatu, Maendeleo ya Jamii pamoja na Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wakati wa Mkutano