Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF YATOA HUDUMA BANDA KWA BANDA

PSSSF YATOA HUDUMA BANDA KWA BANDA

News
News

Dar es Salaam, Julai 8, 2026

Wafanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), wameendesha zoezi la kutembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwa lengo la kuwafikia wanachama wa Mfuko na kuwapatia huduma pamoja na elimu kuhusu hifadhi ya jamii.

Ziara hiyo imewalenga wanachama wa PSSSF ambao, kutokana na majukumu ya kuwahudumia wananchi katika mabanda yao, wamekosa fursa ya kutembelea banda la PSSSF lililopo katika viwanja vya Julius Nyerere.

Afisa wa Mfuko wa PSSSF, Bi. Neema Lowassa (kulia), akimuelekeza namna ya kutumia PSSSF Portal kupitia simu janja, mwanachama wa Mfuko huo wakati tmu ya PSSSF ilipowatembelea wanachama wake kwenye mabanda mbalimbali katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Gerald Minzi, alisema ni utaratibu wa Mfuko panapokuwa na maonesho kuwafuata wanachama walipo ili kuhakikisha wanapata huduma na taarifa muhimu bila kuathiri majukumu yao.

“Tumekuja kuwapatia elimu kuhusu matumizi ya mifumo yetu ya kidijitali, hususan PSSSF Portal, ili muweze kujihudumia popote mlipo bila kulazimika kufika katika ofisi za PSSSF.

Tutawaunganisha na mfumo huo kupitia simu zenu za mkononi ili muweze kupata huduma zetu kwa urahisi, haraka na wakati wowote,” alisema Bw. Minzi.

Afisa wa PSSSF, Bi. Flora Sumari (kushoto), akimuhudumia Mwanachama wa PSSSF kwenye banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati timu ya PSSSF ilipowatembelea wanachama wake ili kuwahudumia kwenye mabanda yao

Miongoni mwa mabanda waliyotembeela ni pamoja na Mabanda ya Halmashauri za Mikoa mbalimbali, banda la Ofisi ya Waziri Mkuu ambalo lina taasisi zote zilizo chini ya ofisi hiyo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na banda la Benki Kuu ya Tanzania, Alisema Afisa kutoka Idara ya FEDHA, PSSSF, Bi.Devota Massawe.

Afisa Matekelezo Mwandamizi Mfuko wa PSSSF, Bw. Gerald Minzi (Kushoto), akimuelekeza Mwanachama wa Mfuko Bw. Moshi Ndimurigo, Katika banda la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam

Akizungumzia faida za matumizi ya huduma za kidijitali, Bi. Massawe, alisema, yanaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za PSSSF, kwa kuwawezesha wanachama kupata taarifa za uanachama, kufuatilia michango na kupata huduma nyingine muhimu kwa urahisi kupitia simu, compyuta au kishikwambi na hivyo kuwezesha kufikia azma ya kaulimbiu ya Tunalipa Jana.