Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF YAIMARISHA USHIRIKIANO NA PDPC KATIKA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

PSSSF YAIMARISHA USHIRIKIANO NA PDPC KATIKA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

News
News

Dar es Salaam, Julai 1, 2026.


Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeendelea kuonesha dhamira yake ya kulinda taarifa binafsi za wanachama na wadau wake kwa kushiriki na kudhamini Kongamano la Kwanza la Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi lililoandaliwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), Dar es Salaam.

Maafisa Matekelezo kutoka PSSSF wakimhudumia na kumpatia maelezo mdau aliyetembelea banda la PSSSF wakati wa maonesho ya Kongamano la kwanza la Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi, kilichofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 01 Julai, 2026.

Kongamano hilo lenye kaulimbiu isemayo "Faragha ya Taarifa kama Nguzo, Usalama na Mustakabali Jumuishi wa Kidijitali kuelekea Dira ya 2050" lililenga kuimarisha uelewa na ushirikiano katika ulinzi wa taarifa binafsi nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Ulinzi Binafsi Dkt. Immanuel Lameck Mkilia akipokea Zawadi kutoka kwa Meneja Matekelezo wa PSSSF Bw. Edger Shimbusho alipo tembelea banda la PSSSF

Alipotembelea banda la maonyesho la PSSSF, Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia alisema “PSSSF ni taasisi yenye hifadhidata kubwa ya taarifa za wanachama wake, na imeendelea kuzihifadhi kwa weledi wa hali ya juu. Tunaipongeza PSSSF kwa kuwa mmoja wa wadau wetu muhimu na kwa ushirikiano wake mkubwa katika kuendeleza utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,"

Mtaalamu kutoka PSSSF akimhudumia na kumpatia maelezo mdau aliyetembelea banda la PSSSF wakati wa maonesho ya Kongamano la 1st Tanzania Annual Data Privacy Conference lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), leo tarehe 01 julai , 2026

Dkt. Mkilia ameipongeza PSSSF kwa kuendelea kuhifadhi taarifa za wanachama kwa viwango vya juu vya usalama na usiri, akieleza kuwa ushirikiano wa taasisi hizo unachangia utekelezaji madhubuti wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na kujenga mazingira salama ya matumizi ya taarifa nchini.

Picha ya pamoja ya Watishi wa PSSSF Katika Kongamano la 1st Tanzania Annual Data Privacy Conference lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), leo tarehe 01 julai , 2026

Ushiriki wa PSSSF katika kongamano hilo unaakisi dhamira ya Mfuko ya kuendelea kuimarisha usalama wa taarifa za wanachama na wastaafu, huku ukiunga mkono juhudi za taifa za kujenga uchumi wa kidijitali ulio salama na jumuishi kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.