Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF: TUTAENDELEA KUTOA HUDUMA BORA NA ZA HARAKA

PSSSF: TUTAENDELEA KUTOA HUDUMA BORA NA ZA HARAKA

News
News

Dodoma, Agosti 8, 2026


Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umewahakishia wanachama na wastaafu kuwa Mfuko huo utaendelea kuboresha na kutoa huduma bora, za haraka na zenye uhakika.


Hayo ameyasema Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Sayi Lulyalya, wakati akitoa shukrani kwa Wanachama, Wastaafu na Wananchi waliotembelea katika mabanda ya PSSSF wakati wa Maonesho ya Klimo na Uvuvi (Nanenane) yaliyofikia kilele Agosti 8, 2026.

Magara Musa Mganga, Afisa matekelezo PSSSF akimuhudumia mwanachama aliyetembelea katika mabanda ya PSSSF wakati wa Maonesho ya Klimo na Uvuvi (Nanenane) yaliyofikia kilele Agosti 8, 2026.


Mgeni rasmi katika sherehe za ufungaji maonesho hayo kitaifa jijini Dodoma alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Aliwashukuru wanachama na wananchi waliotembelea banda la PSSSF katika Maonesho ya Kilimo na Uvuvi (Nanenane) hapa Dodoma, lakini pia Kanda ya Magaribi Mkoani Tabora, Kanda ya Kusini Mkoani Lindi, Kanda ya Nyanda za Juu Mkoani Mbeya, Kanda ya Ziwa Magaribi Mkoani Mwanza, lakini pia Zanzibar." Alisema.

“ Tunathamini mwitikio wa wananchi na wanachama waliotembelea banda la Mfuko na kupata huduma pamoja na elimu kuhusu masuala mbalimbali ya hifadhi ya jamii; Tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora, za haraka na zenye uhakika kwa wanachama na wastaafu," alisema.

Vicky Ishebabi , Afisa matekelezo PSSSF akimuhudumia mwanachama aliyetembelea katika mabanda ya PSSSF wakati wa Maonesho ya Klimo na Uvuvi (Nanenane) yaliyofikia kilele Agosti 8, 2026.


Amewasihi wanachama na wastaafu kuendelea kutumia mifumo ya kidijitali, ikiwemo PSSSF Portal, ili kupata huduma kwa urahisi na kwa wakati bila ulazima wa kufika ofisini.


“ Hivi sasa tumerahisisha upatikanaji wa huduma ikijumuisha Wanachama kupata Taarifa za Mafao, Kuwasilisha madai mbalimbali, Kuhuwisha Taarifa za Wategemezi na Wastaafu nao wanaweza Kujihakiki kupitia simu janja.


Kutokana na kuboresha mifumo yetu PSSSF imeweza kulipa mafao kwa wakati na ndio maana tuna kauli mbiu yetu tunayosema TUNALIPA JANA MSTAAFU WA LEO na kauli hii tunaitekeleza kwa vitendo, alisisitiza Bw. Lulyalya.

Lulu Hussein Bangaseka Afisa Huduma kwa Wateja PSSSF akimuhudumia mwanachama aliyetembelea katika mabanda ya PSSSF wakati wa Maonesho ya Klimo na Uvuvi (Nanenane) yaliyofikia kilele Agosti 8, 2026.