Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
WAGENI 1,600 WATEMBELEA NA KUHUDUMIWA BANDA LA PSSSF MAONESHO YA SABASABA

WAGENI 1,600 WATEMBELEA NA KUHUDUMIWA BANDA LA PSSSF MAONESHO YA SABASABA

News
News

Sabasaba, Julai 14, 2026

Takriban siku 16 za Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) limewahudumia wageni 1,600, Meneja wa PSSSF Kanda ya Ilala Bi. Amina Kassim amesema.

Amesema wageni hao waliojumuisha viongozi wa Serikali, wananchi, wanachama na wastaafu wanaopokea pensheni PSSSF, walipata elimu kuhusu hifadhi ya jamii, huku wanachama na wastaafu wakielekezwa namna ya kutumia huduma za kidijitali kupitia PSSSF Kiganjani na PSSSF Member Portal, alibainisha.

Bi Sylvia Siriwa (kulia) ambaye ni Mstaafu anayepokea pensheni katika Mfuko wa PSSSF, akijihakiki leo Julai 14, 2026, katika banda la Mfuko kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yaliyofikia kilele leo.


“Kupitia mifumo hiyo, wanachama waliwezeshwa kufuatilia taarifa za mafao, kuwasilisha madai, kuhuisha taarifa za wategemezi, kuuliza maswali na kupata taarifa mbalimbali za Mfuko, ikiwemo uwekezaji, kwa urahisi kupitia simu janja.” Alisisitiza Bi. Kassim.

Aidha, wananchi walipata fursa ya kufahamu kwa kina uwekezaji wa PSSSF katika Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi (KLICL), Machinjio ya Kisasa ya Nguru Hills, majengo ya biashara na makazi, pamoja na viwanja vinavyomilikiwa na Mfuko, alisema.

Mnufaika wa Pensheni kutoka PSSSF, John Alex (kulia) akiwa na mama yake Bi. Rosemary akijihakiki kwenye banda la Mfuko katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Julai 14, 226. Katikati ni Bi. Rosemary Peter amabye naye ni mnufaika baada ya kufiwa na mumewe ambaye alikuwa mwanachama wa PSSSF.


Alisema, Maonesho haya yamekuwa jukwaa muhimu la kuonesha mchango wa uwekezaji wa PSSSF katika maendeleo ya taifa. Kupitia banda la Mfuko, wananchi walipata fursa ya kununua nyumba kwa malipo ya papo hapo au kwa utaratibu wa ahadi, kununua bidhaa bora za ngozi zinazozalishwa na KLICL, kama vile viatu, mikoba na mikanda, pamoja na nyama yenye ubora wa kimataifa kutoka Machinjio ya Nguru Hills.

“Uwekezaji huu unaonesha dhamira ya PSSSF ya kuchochea ukuaji wa uchumi, kuongeza uzalishaji, ajira na kuendelea kutoa manufaa ya moja kwa moja kwa wanachama wake na Watanzania kwa ujumla,” alifafanua na kuhitimisha kwa kusema. “Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, tunatoa shukrani za dhati kwa wananchi wote, wanachama, waajiri, wadau na wageni wote waliotembelea banda letu na kushiriki nasi katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Huduma zikiendelea leo Julai 14, 2026