RAIS SAMIA AITUNUKU TUZO PSSSF KWA KUFANIKISHA MDAHALO WA NISHATI SAFI
Zanzibar, Agosti 12, 2026
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa Tuzo kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kutambua mchango wake katika kufanikisha Mdahalo wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, uliofanyika Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, usiku wa kuamkia leo Agosti 12, 2026.

Tuzo ya shukrani iliyotolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF kwa Mchango wa Ushirikiano Katika Kufanikisha Mdahalo wa Nishati Safi ya Kupikia
Mhe. Rais alikabidhi Tuzo hiyo jana kwa Meneja wa PSSSF Zanzibar, Bi. Mariam Saleh ikiwa ni ishara ya kutambua Taasisi zilizoshiriki katika kuwezesha mdahalo huo uliowakutanisha wadau mbalimbali kujadili matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.
Mdahalo huo umefanyika sambamba na Tamasha la 10 la Kizimkazi (Kizimkazi Festival 2026), linalofanyika Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar ambalo limeanza rasmi leo kwa matembezi na uzinduzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Taasisi zilizopatiwa tuzo
Ushiriki wa PSSSF katika mdahalo huo unaakisi jitihada za Mfuko katika kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuleta maendeleo endelevu kwa jamii.