hulipwa kwa mwanachama ambaye anaugua kwa zaidi ya miezi mitatu sababu ya maradhi au ajali kutokana na ajira yake; na hivyo anapokea nusu mshahara. Mwanachama huyo anapaswa awe na umri ulio chini ya umri wa kustaafu kwa hiari na awe amechangia kwenye Mfuko kwa angalau miezi 36.
Iwapo mwanachama atafariki akiwa bado kwenye ajira na amefikisha miezi 180 au zaidi ya uchangiaji; warithi au wategemezi wake watalipwa kiinua mgongo na pensheni ya urithi iwapo wametimiza vigezo (mke/mume na watoto walio chini ya miaka 21). Aidha iwapo mwanachama aliyefariki amechangia chini ya miezi 180 warithi au wategemezi watalipwa malipo maalum ya mkupuo au wastani wa mshahara wa mwaka (APE) kwa kuangalia kiwango kitakachokuwa kikubwa.