Mafao ya kukosa ajira yanatolewa kwa mujibu wa Ibara ya 35 ya Sheria Namba 2 ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ya Mwaka 2018.
Masharti ya Ulipaji wa Mafao ya Kukosa Ajira: -
Nyaraka zinazohitajika:-
Mwanachama atalipwa kila mwezi theluthi moja (33.3%) ya mshahara aliokuwa analipwa wakati ajira yake inakoma. Atalipwa kwa kipindi kisichozidi miezi sita (6). Iwapo atapata ajira kabla ya miezi sita kupita, mafao haya yatasitishwa mara moja i.e. kwa mwanachama aliyechangia chini ya miezi 18, toka alivyolipwa Mafao ya Kukosa Ajira. Mwanachama ana uhuru wa kuomba kuhamisha michango yake kwenda Mpango wa Uchangiaji wa Hiari ambapo anakua huru kuendeleza michango yake au kuomba malipo ya kujitoa kwenye mpango wa hiari.