Mafao hulipwa kwa mujibu wa Ibara ya 33 ya Sheria Namba 2 ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ya Mwaka 2018.
Mafao haya hulipwa kwa Mwanachama aliyeachishwa kazi baada ya kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi kutokana na maradhi, ulemavu wa mwili au akili kama itakavyothibitishwa na jopo la madakatari
Awe na ulemavu au maradhi ambayo hayajatokana na ajira yake (wanaopoteza uweza wa kufanya kazi kutokana na ajali au maradhi yatakanayo na ajira zao hulipwa chini ya mpango wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mafao haya hulipwa kwa sehemu mbili, ambazo ni malipo ya mkupuo na pensheni ya mwezi kwa kipindi chote cha uhai wa mwanachama iwapo amechangia kipindi cha miezi isiyopungua miezi thelathini na sita (36) na kati ya hiyo, miezi kumi na mbili (12) ya mwisho iwe na michango.
Masharti ya ulipaji wa Mafao ya Ulemavu:-
Awe Mwanachama wa Mfuko wa PSSSF
Awe chini ya umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55),
Awe amechangia kwenye Mfuko angalau miezi 36 ambapo kati ya hiyo miezi 12 iwe imechangakiwa kabla ya ugonjwa
Ili Mwanachama aweze kunufaika na Mafao ya Ulemavu atalazimika kuwasilisha fomu PS-BEN.3 ikiwa imejazwa vyema ikiambatana na nyaraka zifuatazo:-
Barua au taarifa ya kustaafu kwa sababu za ulemavu kutoka kwa mwajiri
Fomu ya tiba PS-BEN.5 (ripoti ya jopo la madaktari),
Barua ya Mwanachama kuomba mafao ya majumuisho kabla ya kulipwa na Mfuko wowote (kwa Mwanachama aliyechangia zaidi ya Mfuko mmoja)
Nakala ya kadi ya benki iliyokuwa ikipitisha mshahara,
Nakala ya kadi ya benki iliyokuwa ikipitisha mshahara,
Nakala ya kadi ya benki iliyokuwa ikipitisha mshahara,
Nakala ya Kitambulisho cha Taifa/Leseni ya Udereva/ Hati ya Kusafiria/ Kitambulisho cha Mpiga Kura,