• Tupigie bure: 0800 110040
   
single-img-three
single-img-four
single-img-five
Mfuko Wa Hifadhi Ya Jamii Kwa Watumishi Wa Umma

Kutoa huduma bora ya hifadhi za jamii kwa watumishi wa Umma

Serikali kupitia Sheria namba 2 ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma mwaka 2018, ilifuta Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya LAPF, PSPF, GEPF, PPF na kuanzisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).Hivyo kuanzia tarehe 1 Agosti, 2018 waliokuwa wanachama wa Mifuko iliyounganishwa yaani LAPF, PSPF, GEPF na PPF walihamishiwa katika Mfuko wa PSSSF na wataendelea kuwa wanachama na kuchangia katika Mfuko (isipokuwa wanachama wote waliokuwa watumishi wa sekta binafsi kutoka Mifuko iliyounganishwa walihamishiwa NSSF, na watumishi wa Umma waliokuwa NSSF walihamishiwa PSSSF kuanzia Februari, 2019).
  • Wanachama wa Mfuko ni wastaafu na wategemezi waliokuwa wanalipwa pensheni na Mifuko iliyounganishwa pamoja na Watumishi waliajiriwa kuanzia tarehe 1 Agosti, 2018 katika sekta ya Umma pamoja na makampuni yote ambayo Serikali inamiliki hisa za zaidi ya asilimia thelathini (30%).
  • Mafao yatolewayo na Mfuko ni Mafao ya muda mrefu na Mafao ya muda mfupi. Mafao ya muda mrefu ni; Mafao ya Uzeeni, Mafao ya Ulemavu, Mafao ya Kifo na Mafao ya Wategemezi. Kwa upande wa mafao ya muda mfupi ni; Mafao ya Kukosa Ajira, Mafao ya Ugonjwa na Mafao ya Uzazi.
  • Shughuli za uwekezaji za Mfuko zinafanywa kwa mujibu wa ibara ya 53 ya sheria namba 2 ya PSSSF. Uwekezaji unatekelezwa kwa mujibu wa sera ya uwekezaji ya Mfuko/miongozo/kanuni za Benki Kuu na Wizara yenye dhamana ya sekta ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajiea na Wenye Ulemavu). Mfuko unapokusanya michango kutoka kwa wanachama na waajiri huiwekeza ili kulinda thamani ya fedha na kuuwezesha Mfuko kumudu majukumu ya ulipaji mafao.
  • Mfuko umerahisisha huduma kwa wanachama kwa kuwa na; kituo cha huduma kwa wateja, dawati la malalamiko katika ofisi zote, mitandao ya kijamii na tovuti, huduma za PSSSF kiganjani, PSSSF popote ulipo mtandaoni na Pamoja App, elimu kwa wanachama kupitia semina na matangazo.
  • Mfuko una ofisi Tanzania nzima na zimegawanyika katika kanda zifuatazo; Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kati, Kanda ya ziwa magharibi, Kanda ya nyanda za juu kusini, kanda ya mashariki, kanda ya Ilala, Kanda ya Kinondoni, Kanda ya Temeke na ofisi ya Zanzibar.

Sema na sisi

PSSSF inawahimiza kuwasilisha taarifa za tabia zisizo za kiadilifu zinazofanywa na watumishi wake au washirika wake zinazohusisha Mfuko ambazo zinaweza kuwa na athari kwa wanachama au wastaafu. Tunawahimiza kuwasilisha taarifa hapa, na Mfuko utachukua hatua stahiki kulingana na taarifa zinazotolewa. Taarifa hizi zinajumuisha udanganyifu, rushwa, unyanyasaji, wizi, n.k.
PSSSF ina furaha kutambulisha njia mbadala za kuwasilisha maoni na kushughulikia malalamiko, ambazo zitasaidia kuboresha huduma kwa wateja wetu wa thamani. Iwapo haujaridhika na huduma zetu, tafadhali jisikie huru kutoa maoni yako. Kwa maelezo zaidi, tafadhali rejea taratibu zetu za kushughulikia maoni maoni na malalamiko kwa kubofya hapa.
Mitandao ya Kijamii ya PSSSF kama vile Facebook, Twitter, YouTube, na Instagram inasimamiwa na watumishi wa Mfuko. Mfuko hauhusiki na maudhui yanayotengenezwa na tovuti za nje.
Taarifa hizi zinazotolewa na PSSSF zinalenga kutoa elimu kwa wanachama wa PSSSF pekee na hazitumiwi kwa madhumuni ya biashara au faida ya aina yoyote ya kifedha kwa namna yoyote ile.