PSSSF yatengeneza post mpya

Katika kuboresha huduma zetu PSSSF imekuja na mambo mazuri kwa mwanachama wak

*Awataka watekekeleze wajibu wao kwa kasi huku wakizingatia sheria

*Wasiwe chanzo cha kukwama kwa zabuni

*DPS: Tutatekeleza majukumu kwa weledi,kasi na kuzingatia sheria

Na Mwandishi Maalum, Arusha

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumsihi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba amewataka watumishi wa Kurugenzi wa Ununuzi na Ugavi ya PSSSF kutokuwa chanzo cha kukwama kwa zabuni mbalimbali za Mfuko.

CPA. Kashimba alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akifungua kikao kazi cha Kurugenzi ya Ununuzi na Ugavi kilichofanyika jijini Arusha Februari 24,2023.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba akihutubia wakati akifungua kikao kazi cha Kurugenzi ya Ununuzi na Ugavi

“Nawapongeza kwa kazi mnazofanya kwa kuhakikisha kazi za Mfuko hazikwami. Hata hivyo katika utekelezaji wa majukumu yenu hakikisheni mnazingatia weledi na muda uliowekwa kwa kila zabuni kukamilika” alisema CPA. Kashimba.

Mkurugenzi Mkuu, alisema Kurugenzi ya Ununuzi na Ugavi ni muhimu sana katika utendaji wa kila mtu katika Mfuko, hivyo aliwataka waendelee kujipanga vyema ili isitokee hata siku moja wakakwamisha utendaji wa Kurugenzi nyingine ndani ya Mfuko.