
PIC: Mradi wa PSSSF Oloirieni ni Mfano, sasa unavuna faida
Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Augustine Vuma Holle (wa pili kulia) akiongoza waheshimiwa wabunge wajumbe wa kamati hiyo kutembelea mradi wa nyumba za makazi wa Oloirieni uliopo jijini Arusha unaomilikiwa na PSSSF,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru
*Unaliletea taifa heshima
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kusimamia vyema mradi wa nyumba za makazi wa Oloirieni uliopo jijini Arusha ambao unaendelea kuvuna faida kwa PSSSF na kuufanya Mfuko uweze kutekeleza vyema majukumu yake.
Kauli hiyo imetolewa jijini Arusha na mwenyekiti wa PIC, Mhe. Augustine Vuma Holle wakati wa kikao cha majumuisho baada ya kamati hiyo kutembelea mradi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru akitoa taarifa ya utekelezaji mbele ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ilipotembelea mradi wa nyumba za makazi wa Oloirieni uliopo jijini Arusha unaomilikiwa na PSSSF.
“Kamati imeridhishwa na mradi huu, mradi huu ni mradi wa mfano, hili ni jambo jingine uwekezaji mkubwa na wa kisasa, hakika eneo hili kwa ubora wake linatuaheshimisha kama taifa. Pia kamati inaelekeza kuwe kunafanyika ukarabati wa mara kwa mara kwenye mradi huu na PSSSF ifatilie wadaiwa sugu” alisema Mwenyekiti huyo wa PIC.
Kwa upande wake makamu Mwenyekiyi wa kamati hiyo, Mhe. Mary Masanja alisema, “Kazi nzui inaonekana wazi,kubwa ambalo mimi nimeliona ni jinsi mradi huu ulivyotoa fursa kwa watu mbalimbali kufanyakazi ambazo zinawaingizia kipato, hongereni sana”.
Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Augustine Vuma Holle akitoa maelekezo ya kamati wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa nyumba za makazi wa Oloirieni uliopo jijini Arusha unaomilikiwa na PSSSF.
Naye, Mhe. Abbas Tarimba, Mbunge wa Kinondoni na mjumbe wa kamati hiyo alisema, “mradi huu ni wa mfano kwani uwekezaji huu umeshaanza kulipa na sasa PSSSF inavuna faida, hata hivyo ili kuongeza thamani ya eneo hili ukarabati zaidi unatakiwa ili thamani iongezeke na Mfuko kuingiza fedha zaidi”.
Mwakilishi wa katibu Mkuu katika ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Festo Fute alisema wamepokea maelekezo yote tayari kwa kuyafanyia kazi mara katika kuhakikisha mradi unaendelea vizuri.
Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa mradi wa nyumba za makazi wa Oloirieni uliopo jijini Arusha unaomilikiwa na PSSSF, Bw. Muro
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru alisema, “Tutaendelea kuboresha mradi huu ili uendelee kuwa bora zaidi, pia tumejipanga kujenga mradi mkubwa na wa kisasa jijini Dodoma ambao utapendezesha jijini la Dodoma, mradi utajulikaa kama mradi wa Njedengwa.”
Gharama ya mradi huo uliozinduliwa mwaka 1998 hadi kukamilika kwake zilikuwa shilingi bilioni 13.29, na hadi kufikia mwaka 2012 gharama ya mradi huo zilikuwa zimerejeshwa. Hivyo kuanzia wakati huo hadi sasa Mfuko unaendelea kuvuna faida.