PSSSF Yamuaga Bakari Machumu Anayemaliza Muda Wake Kama Mkurugenzi wa MCL
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa PSSSF Ndg. Paul Kijazi (watatu kushoto) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communication ltd (Shirika la Magazeti la Mwananchi) Ndg. Bakari Machumu (katikati) katika picha ya pamoja na maafisa wa PSSSF walimpomtembelea Ndg. Machumu leo katika ofisi zake leo, jijini Dar es Salaam.
* Hongera kwa Utumishi wako na mchango mkubwa katika Tansia ya Habari nchini.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umemtembelea Bw. Bakari Machumu, Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), kwa lengo la kutambua mchango wake mkubwa katika sekta ya habari na mawasiliano. Ziara hiyo, iliyofanyika tarehe 22 Agosti 2024, iliwapa fursa wajumbe wa PSSSF kumpongeza Bw. Machumu kwa utendaji wake kipindi chote alipokuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL lakini pia kwa mchango mkubwa katika Tansia ya Hbarai, Tanzania.
kuwasilisha zawadi maalum kwa niaba ya uongozi wa i.
Bw. Bakari Machumu, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magazeti la Mwananchi (MCL) akizungumza na maafisa wa Mfuko wa PSSSF wakiongozwa na Bw. Paul Kijazi, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa PSSSF wakati wa ziara hiyo.
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Paul Kijazi, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa PSSSF, aliongoza maafisa wa PSSSF kwenda kumuaga Bw. Machumu na kumshukuru kwa utumishi wake katika tansia ya habari,
PSSSF walimkabidhi zawadi Bw. Machumu kama ishara ya shukran, akieleza heshima kubwa ambayo Bw. Machumu amejenga kutokana na uongozi wake thabiti katika kuimarisha tasnia ya habari nchini Tanzania.
Uphoo Swai, Meneja wa Makao Makuu Ndogo ya PSSSF, pamoja na maafisa wengine waandamizi, walikuwepo kushuhudia tukio hilo na kumtakia Bw. Machumu mafanikio katika hatua zake zijazo za maisha.
Bw. Bakari Machumu akizungumza na Bw. Paul Kijazi, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa PSSSF walipomtembelea Bw. Machumu ofisini kwake Mwananchi Communication Limited, leo tarehe 22/08/2024, Dar es Salaam.
Bw. Kijazi alimpongeza Bw. Machumu kwa uongozi wake madhubuti na juhudi zake za kuboresha viwango vya uandishi wa habari nchini. Alisisitiza kuwa MCL imefikia mafanikio makubwa chini ya uongozi wake na kumtakia kila la heri katika shughuli zake zijazo, akiongeza kuwa mchango wake utaendelea kukumbukwa na kuthaminiwa kwa muda mrefu.
Bw. Bakari Machumu, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magazeti la Mwananchi (MCL) wakifurahia jambo na maafisa wa PSSSF na baadhi ya menejimenti ya Mwananchi Communication ltd.
Bw. Mpoki Thomson, Mhariri Mtendaji gazeti la The Citizen (katikati) akizungumza na maafisa wa PSSSF (hawapo pichani) walipotembelea ofisi za Mwananchi Communication Limited, jijini Dar es Salaam, Kulia ni Bw. Victor Mushi, Mhariri Mtendaji Mwananchi Communication Limited na kushoto ni Bw. Edson Sosthenes.
Mwisho.
Latest News
- PSSSF Yamuaga Bakari Machumu Anayemaliza Muda Wake Kama Mkurugenzi wa MCL
- PSSSF YATOA TZS MILIONI 10, KUSAIDIA TIBA KWA WATOTO WENYE MARADHI YA MOYO
- Bunge lampongeza Mhe. Rais SSH kwa kuilipa madeni ya muda mrefu ya PSSSF
- PSSSF Management Meeting
- Hon. Ndejembi Meets with PSSSF Management
- PSSSF Digital Systems to Increase Transparency in Service Delivery: Minister Ndejembi
- PSSSF RUNS ‘BANDA KWA BANDA’ CAMPAIGN TO EDUCATE MEMBERS ON THE USE OF DIGITAL FORM
- PSSSF participates in Sabasaba to support Government Efforts in Business
- PSSSF Fire Wardens Attend Intensive Training at Tanzania Fire and Rescue Force
- HON. MINISTER SIMBACHAWENE PRAISES PSSSF TECHNOLOGICAL REFORMS IN DODOMA JUNE 19, 2024