PSSSF yawanoa Jeshi la Polisi Tanzania jinsi ya kuwasilisha nyaraka kidijitali
Bw. Mbaruku Magawa akitoa elimu ya matumizi ya mtandao wa kuwasilisha fomu za madai ya mafao na kujiunga kwa wanachama wapya kwa Kamishna wa Kamisheni ya Utawala na Rasikimali Watu CP. Suzan Kaganda wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa Maafisa wake jijini Dar es Salaam, tarehe 14 Mei, 2024.
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Utumishi wa Umma (PSSSF) umeendesha mafunzo ya namna ya kuwasilisha madai kupitia mifumo ya ICT kwa maafisa wa Dawati la Mafao wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Akizungumza katika hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Tanzania IGP Carmilius Wambura, CP Suzanne Kaganda alisema mfumo wa kuwasilisha nyaraka utasaidia wanachama kufuatilia madai yao wenyewe kwa haraka na uwazi. "Ninawahimiza kutumia fursa hii ya kipekee, kuwa wepesi kujifunza ili muweze kwenda na kasi ya teknolojia."
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Abdu-Razaq Badru akielezea maono yake ya baadae kuhusu PSSSF ya Kidijitali wakati wa akitoa salamu wakati wa semina ya elimu kwa Jeshi la Polisi, Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika kumbi za PSSSF Golden Jubilee Tower.
Akitoa salamu kwa niaba ya PSSSF, Mkurugenzi Mkuu, Bwana Abdul-Razaq Badru alisema PSSSF imetehemisha operesheni zake ili kuboresha huduma kwa wanachama na wadau. "Jeshi la Polisi ni moja ya makundi maalum yanayohudumiwa na PSSSF kwa kutumia huduma zetu za kidijitali, tunajitahidi kutoa huduma sahihi na kuondoa mnyororo wa utoaji huduma."
DCP Seniono akuzungumza na kutooa salamau wakati wa semina ya elimu kwa Jeshi la Polisi, Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika kumbi za PSSSF Golden Jubilee Tower.
DCP Gabriel Semiono alishukuru PSSSF akisema "hii ni hatua muhimu kwani sasa tunatoa huduma kwa maafisa wetu pale walipo badala ya kufunga safari kwenda Makao Makuu ya Polisi."
Baadhi ya Maafisa wa Mfuko wakitoa semina kwa Maafisa wa Polisi wakati wa semina ya elimu kwa Jeshi la Polisi, Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika kumbi za PSSSF Golden Jubilee Tower.
Mafunzo kwa maafisa wa Polisi yanakusudia kuleta ufanisi na uwazi katika kudai mafao kupitia njia za kidijitali. Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha wanachama wanapokea mafao yao kwa wakati na kwa ufanisi.
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Polsi katiak semina