
Karibu Abdul-Razaq Badru, kwaheri CPA. Kashimba
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Abdul-Razaq Badru.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Abdul-Razaq Badru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Badru alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Februari 6, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Bi. Zuhuru Yunus, ilisema uteuzi wa Bw. Badru unaanzia Februari 6, 2024 akichukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Bw. Badru alizaliwa Aprili 3, 1968 ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 ya kufanyakazi katika taasisi za umma na binafsi, amefanyakazi kwa mafanikio katika miradi iliyo chini ya Shirika la Maendeleo la Uingereza DFID, Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Benki ya dunia.
Mkurugenzi mkuu Badru ana shahada ya uzamili katika Internatinal Business Management kutoka Indian Insitute for Foreign Trade, ana shahada ya Sosholojia kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia ana Postgraduate Diploma in Leadership kutoka Aalto University Executive Education cha Finland na Uongozi Leadership Institute cha Tanzania.
Ni Mkurugenzi anayetambuliwa na Institute of Directors cha Tanzania (IDoTZ), na mjumbe katika bodi mbalimbali ikiwemo STAMICO, KCMCo, BOT-Mwalimu Nyerere Memorial Scholarship, SUA-mjumbe wa kamati ukaguzi na hadhari. Pia Bw.Badru ni katibu wa umoja wa Watendaji Wakuu wa taasisi za umma tangu mwaka 2017.