
Katibu Mkuu Luhemeja atembelea PSSSF
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja katika picha ya pamoja na Menejimenti ya PSSSF
Katibu Mkuu Luhemeja atembelea PSSSF
Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi Cyprian Luhemeja, amefanya ziara ya kiutendaji katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).Katika Zaira hiyo, Mhandisi Luhemeja ameelekeza Menejimenti ya PSSSF, kuendelea kutoa elimu kwa umma ili Wananchi waweze kujionea kazi kubwa ambayo imefanyika toka kuunganishwa kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, PPF, GEPF na LAPF.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja katika kikao kazi na Menejiment ya PSSSF Makao Makuu Ndogo ya Mfuko, jijini Dar Es Salaam.
"Kazi kubwa na nzuri imefanyika kwa kipindi cha miaka mitano toka kuunganishwa kwa Mifuko hiyo, utendaji umeboreshwa kwa kiasi kikubwa, ni muhimu watanzania waweze kuelewa kazi ambayo Serikali inafanya kwa niaba yao" alisema Mhandisi Luhemeja.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, amesema kwamba tokea kuunganishwa kwa Mifuko, uhai wa PSSSF sasa unaonekana, kwani imeweza kulipa madeni yote iliyorithi toka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya awali na ukuaji umefikia kiasi cha Trillioni 8. "Gharama ya uendeshaji imepungua kwa asilimia 50, jambo ambalo limeboresha utendaji kwa kiasi kikubwa" alisema CPA Hosea Kashimba.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemejaakipokea zawadi kutoka Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba baada ya kikao kazi.