
Dkt. Biteko Akutana na Mkurugenzi Mkuu PSSSF
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba, bungeni jijini Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba (wa pili kulia), katika ofisi ya Naibu Waziri Mkuu leo Novemba 3, 2023 Bungeni jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Bw. James Mlowe (wa pili kushoto) na Bw. Abdul Njaidi wa PSSSF.
CPA. Kashimba alipata fursa ya kumpongeza Dkt. Biteko kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo Agosti 30, 2023 na kula kiapo Septemba 1, 2023.
Pia CPA. Kashimba alitumia fursa hiyo kujitambulisha ikiwa ni pamoja na kumueleza utekelezaji wa majukumu ya Mfuko kama yalivyoainishwa kwenye Sheria namba 2 ya mwaka 2018 iliyoanzisha PSSSF, ambayo ni pamoja na kuandiskisha wanachama, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Bideko (katikati), akipokea mfuko wenye taarifa mbalimbali kuhusu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, ofisini kwa Naibu Waziri Mkuu kwenye ofisi za Bunge jijini Dodoma, Novemba 3, 2023. PSSSF iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Kulia ni Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, PSSSF, Bw. James Mlowe.
PSSSF, ni miongoni mwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.