• Waziri Mkuu atembelea banda, avutiwa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambao ni wabia pamoja na Jeshi la Magereza katika uendeshaji wa kiwanda cha Karanga Leather Industries Co Ltd (KLICL) cha kutengeneza bidhaa za ngozi wameshiriki maonesho ya viwanda ya SADC. 

Maonesho hayo yaliyoanza Jumatatu Agosti 5, 2019 yalikuwa na kauli mbiu ya Mazingira Wezeshi ya Biashara Kwa Maerndeleo Jumuishina Endelevu ya Viwanda, washiriki wa maonesho hayo wametoka nchi wanachama wa SADC.

1

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alitembela banda ya kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga na kuridhishwa na utendaji kazi wa kiwanda hicho. PSSSF imeingia ubia na Jeshi la Magereza kwa lengo la kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda kwa vitendo.

Faida zinatorajiwa kutokana na uwekezaji katika kiwanda cha bidhaa za ngozi Karanga ni pamoja na; Kupatikana kwa soko la uhakika la ngozi ghafi kutoka kwa wafugaji, Kuongezeka thamani ya ngozi inayozalishwa nchini, Kuongezeka kwa uzalishaji wa ngozi ghafi na bidhaa za ngozi na kuongeza ajira ambapo kutakuwa na ajira za moja kwa moja mpaka wafanyakazi 3000 na zaidi ya ajira 4000 kutokana na shughuli za uzalishaji.

2

Karanga Leather Industries Co Ltd (KLICL) ilianzishwa tarehe 30 Mei, 2017 kwa lengo la kutekeleza mradi wa viwanda vya bidhaa za ngozi katika eneo la Gereza la Karanga, Moshi, Kilimanjaro. Kampuni hii ilianzishwa kwa ubia kati na Mfuko wa PSSSF pamoja na Jeshi la Magereza.